Vijana Leo

UTUME KWA VIJANA 1
Sahaya G. Selvam, SDB
Hali ya Vijana wa Siku Hizi: Ukweli na Uwongo
 
“Vijana wa siku hizi… hatuelewani nao!  Kizazi hiki kimepotea!  Dunia imechafuka!”  Malalamiko ya watu wazima kuhusu vijana ndiyo haya.  Hata vijana wanaweza kukubali kirahisi na sentensi zifuatazo:
 

Vijana wanaonekana kuwa waasi.
Vijana wa siku hizi hawajali dini.
Vijana hawaelewani na wazazi wao.
Vijana wanapendelea zaidi kusoma makala za burudani, vitabu vya hadithi (riwaya) na kutazama TV na Filamu.
Asilimia kubwa ya vijana wa mijini hawajijali, na hutumia madawa ya kulevya.
Vijana wa siku hizi wanapenda kupiga kelele nyingi, wakorofi, na wasumbufu.
Vijana wanatarajia kupata burudani tu kutoka kwenye vituo vya vijana.
Vijana siku hizi wanakosa maadili na msimamo wa […]

Continue reading


Yesu na Utume kwa Vijana

UTUME KWA VIJANA 2
Sahaya G. Selvam, SDB
Yesu : Mfano Bora wa Utume kwa Vijana

 

Vijana wenyewe si matatizo, bali wanaweza kuwa na matatizo.  Ni wajibu wa wanakanisa kuwasindikiza vijana na kuwasaidia ili wenyewe watatue matatizo yao. Huu ndio utume kwa vijana.  Aliyetoa mfano mzuri kwa utume huu kwa vijana ni Yesu mwenyewe.  Katika makala hii tutafakari jinsi Yesu mwenyewe alivyowasaidia vijana wawili, waliokuwa wamekata tamaa, kujenga matumaini na wenyewe kuwa mitume kwa vijana (wafuasi) wengine.
Tunapata mfano huu katika tukio la “Safari ya Kwenda Emau” (Lk 24:13-35)
 
Siku hiyohiyo, wawili kati ya wafuasi wake Yesu wakawa wanakwenda katika kijiji kimoja kiitwacho Emau, umbali wa kilomita kumi na moja kutoka Yerusalemu.  Wakawa wanazungumza juu ya hayo yote yaliyotukia. (Lk 24: 13-14, Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa.)
 
Ningependa kufikiria kwamba hawa wafuasi wawili walikuwa vijana.  Kadiri ya Sera ya Maendeleo ya Vijana katika nchi nyingi kama Tanzania, kijana ni mtu yeyote mwenye umri ya miaka […]

Continue reading


Malezi Jumla

UTUME KWA VIJANA 3
Sahaya G. Selvam, SDB
Malezi jumla kwa Vijana
 
Naye Yesu Akakua…
 
Mtoto Yesu alipoanza kuingia katika ujana wake, akiwa na umri wa miaka kumi na miwili, alianza kutafuta maana ya maisha yake.  Alitaka uhuru zaidi kutimiza malengo ya maisha yake.  Ndiyo maana alikuwa amepotea hekaluni. Alianza kutambua kwamba ilikuwa inampasa kuwa katika nyumba ya Baba yake!  Lakini mwinjili Luka anatuambia kwamba baada ya wazazi wake kumwona,
“Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii…. Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima, na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu.” (Lk 2:51-52)
Nafsi ya kila binadamu ina vipengele vinne.  Hivi ni Mwili, Akili, Hisia (Moyo) na Roho. Vipengele hivi vinaendana na mahitaji manne makuu ya binadamu.  Sisi binadamu tunataka kuishi; tunatafuta usalama na raha ya kimwili.  Ya pili, tunataka kujifunza mambo mapya, yaani kukuza akili zetu.  Ya tatu, daima binadamu hutafuta uhusiano na watu; tunataka kuwapenda watu na kupendwa na watu; ndiyo haya mahitaji […]

Continue reading


Mabadiliko ya Tabia

UTUME KWA VIJANA 4
Sahaya G. Selvam, SDB
 
Namna ya Kuwafundishia Vijana ili
Kuleta Mabadiliko ya Tabia
 
“Semina, semina, semina! Nimechoka na semina hizi!”, kijana mmoja alinilalamikia mara baada ya kurudi kutoka Kongamano la Pasaka.
Nilikuwa ninaongea na Askofu wa jimbo moja la Tanzania, na nikamwambia, “Baba askofu, nimesikia kwamba asilimia kubwa ya vijana wa mkoa huu wameathirika na ukimwi, kama kanisa tumefanya nini kukabiliana na hali hii?”  Akanijibu mara moja kwa uhakika, “Tumefanya semina nyingi tu!”
Semina, semina, semina! Je, semina hizi huleta mabadiliko ya tabia? Au semina hizi ni njia mojawapo ya kula misaada tunayoipata kutoka nchi za nje badala ya kukabiliana na matatizo ya kijamii kama ukimwi?
Hakika, zipo njia nyingi tu za kutoa malezi kwa vijana, baadhi zake nimekwisha kuzitaja katika toleo lililopita.  Licha ya michezo na vitendo mbalimbali katika vikundi, njia kubwa ya kutoa malezi kwa vijana ni kwa njia ya mafundisho darasani, semina na warsha.  Katika makala hii, ningependa […]

Continue reading


Familia na Vijana

UTUME KWA VIJANA 5
Sahaya G. Selvam, SDB
 
Kuwawezesha Vijana Kujenga Familia za Kikristu
 
“Kizazi hiki kimepotea. Vijana wa siku hizi hawana msimamo.  Kuna mmomonyoko wa maadili….” Haya ndiyo malalamiko tunayosikia kutoka kwa watu wazima.  Ukweli ni kwamba, tuwaleavyo vijana ndivyo wakuavyo! Hali ya vijana wa siku hizi ni matokeo ya hali ya familia zetu.  Na hali ya familia zetu si ya kujivunia.
 
Padre Shorter, mtaalamu wa mambo ya kijamii na kitamaduni, analalamika, “Katika jamii za Afrika siku hizi, mfumo wa familia umeathiriwa na mabadiliko ya kijamii na kimila.  Taratibu za jando na unyago zimeanza kupotea. Malezi kuhusu maisha ya kifamilia hayatolewi nyumbani wala shuleni.  Hivyo, vijana wamepoteza msimamo wao, nao kujiingiza katika mapenzi ovyo.” (African Culture: An Overview, 1998, p.95)
 
Mimi naamini kwamba ili kugeuza hali ya familia zetu kuna njia moja tu: inatubidi tuanze na vijana wetu.  Ingawa wengi wao wanatokea familia zilizobomoka, wanaweza kuzuia hali hii isiendelee zaidi.  Wanahitaji kuwezeshwa kuamua […]

Continue reading