Lectio Divina

UTUME KWA VIJANA 12
Sahaya G. Selvam, SDB
 
Lectio Divina Kwa Vijana
 
Tangu mwaka 1985, imekuwa desturi katika Kanisa Katoliki kuadhimisha Jumapili ya Matawi kuwa Siku ya Vijana Duniani. Aidha, kila mwaka katika adhimisho hili Baba Mtakatifu huwa anatoa ujumbe maalumu kwa ajili ya vijana duniani kote.  Hata mwaka huu wa 2006, katika adhimisho la 21 la Siku ya Vijana Duniani (9 April 2006), Baba Mtakatifu ametoa ujumbe kwa vijana wote: “Dhamira ninayopendekeza kwenu ni kutoka Zaburi 119: 105 –  “Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu.”
 
Katika ujumbe wake anasisitizia kuwa vijana wa siku hizi tunaishi katika mazingira magumu yenye falsafa za uongo na maadili potofu.  Katika mazingira haya ya giza Neno la Mungu ndilo linaloweza kuiangaza njia yetu.
 
Papa anatukumbushia maneno ya mwandishi wa Waraka kwa Waebrania anayesema: “Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo […]

Continue reading


Vijana na Tabia hatari

UTUME KWA VIJANA 13
Sahaya G. Selvam, SDB

Sababu za Vijana Kujingiza katika Tabia za Hatari
na Namna ya Kuwasaidia
 
Katika makala hii tunashirikisha namna ya kuwasaidia vijana ili waweze kuvuka vikwazo vinavyoweza kuwafanya wasifikie malengo waliojiwekea maishani mwao. Tunatambua kwamba, yapo mambo mengi yanayoweza kuwachelewesha au kuwakwaza vijana kutofikia malengo yao ya maisha. Baadhi yake ni kama:

Dawa za kulevya
Ulevi
VVU/Ukimwi
Mimba kabla ya wakati,  n.k.

 
Katika makala hii, tunaelezea sababu chache zinazopelekea vijana (wasichana) kupata mimba kabla ya wakati. Pia tunapendekeza namna ya kuweza kuwasaidia ili wasijikute katika mtego huu na pia waweze kufikia malengo yao katika maisha yao. Ingawa sababu hizi zinawalenga wasichana moja kwa moja, hata hivyo zinaweza kutumika kwa wavulana pia, kwa vile wavulana wanajiingiza katika mambo haya kirahisi kuliko wasichana.
 
Bi. Tricia M. Davis amefanya utafiti kati ya wasichana wapatao 500 wenye umri wa miaka chini ya 19, waliowahi kupata mimba zaidi ya mara moja. Katika utafiti wake anaeleza sababu saba […]

Continue reading


Spoti na Utume kwa Vijana

UTUME KWA VIJANA 14
Sahaya G. Selvam, SDB

Spoti na Utume kwa Vijana
 
Ujana ni kipindi katika maisha ya binadamu chenye nguvu nyingi.  Spoti ni mkondo mzuri wa kutumia nguvu hii, na pia njia nzuri ya kujiburudisha kwa vijana.  Burudani ina sehemu yake muhimu katika maisha ya binadamu ili tuwe na afya ya kimwili na ya kiakili.  Ndiyo maana binadamu anaitwa homo ludens, yaani, binadamu mchezaji!  Anapotumia nguvu yake kwa ajili ya kutafuta riziki, hii ni kazi; lakini anapofanya mambo ya burudani na ubunifu bila kutafuta faida yoyote, huu ni mchezo.
 
Basi, katika makala hii ningependa kushirikisha nanyi mawazo machache kuhusu spoti na utume kwa vijana.  Yaani, jinsi michezo, hasa spoti, inaweza kutumika vizuri katika malezi ya vijana. (Michezo kwa ujumla inaweza kumaanisha hata ngoma na tamthilia, lakini spoti ni michezo inayofanyika uwanjani na kuwapa watu nafasi ya kukimbia na kuvinyosha viungo vya mwili.)  Michezo ni njia nzuri ya kuwavutia vijana katika mazingira […]

Continue reading


Vijana na Dini

UTUME KWA VIJANA – 15
Sahaya G. Selvam, SDB
Vijana na Dini
Ilikuwa Jumapili asubuhi.  Nilikuwa najiandaa kwenda kwenye ibada, simu yangu ya mikononi ikalia.  Kulikuwa na sms kutoka msichana mmoja ambaye aliwahi kuwa mwanafunzi wangu katika Chuo Kikuu.  Ujumbe ukasema, “Padre, sijisikii kwenda kwenye misa leo.  Nataka kwenda.  Je, unaweza kunipa sababu tatu ili kunimotisha kwenda kanisani?”  Nikampa sababu moja tu, “Yesu anakusubiri!”  Basi, hatimaye akaenda!
 
Barani Afrika kati ya washiriki wa ibada za kanisani bado wengi ni vijana.  Vyama vya vijana viko hai sehemu nyingi, na vijana wanachangia kiasi kikubwa katika kuboresha liturjia, kwa njia ya kuimba na kucheza ngoma za kiliturjia. Je, vijana kweli wanajisikia nyumbani katika kanisa?  Je, kanisa linatimizia kweli mahitaji ya vijana? Je, mambo ya dini ni kwa ajili ya wazee tu?   Na kwa nini baadhi ya vijana wamekuwa watalii wa kidini – yaani wanapenda kutembelea makanisa mengi kuonja mahubiri na liturjia tofauti tofauti?  Katika makala hii tujitahidi […]

Continue reading


Katekisimu kwa ajili ya Vijana – 1

UTUME KWA VIJANA – 16
Sahaya G. Selvam, SDB
Katekisimu kwa ajili ya Vijana – 1

Utangulizi:
Kutokana na uzoefu wangu wa kutoa semina na mafungo kwa ajili ya vijana katika nchi za Afrika Mashariki nimeona kuwa vijana wengi wana maoni kuhusu imani ya kikristu ambayo ni hafifu.  Wengine wana msimamo wa kikristu ambao unawabana mno, hata wanaona hawawezi kuwa wakristu wakamilifu.  Wengi wanaishi na mgogoro kati ya imani iliyo kali na maadili ya kujiruhusu mno. Kutokana na katekesi potofu vijana wengi wana msimamo wa zamani, au msimamo ambao hauendani na mafundisho rasmi ya kanisa la sasa.  Kwa ujumla, uelewa wa imani yao haujakua kadiri ya ukuaji wa umri na maendeleo ya historia ya dunia na kanisa.
Katika makala hii basi, ningependa kutoa kwa mtindo wa maswali na majibu mawazo machache yanayoweza kuleta picha ya ukristu yenye furaha na uhuru.  Yesu alisema nimekuja ili muwe na uhai, tena uhai tele (Yn 10:10).  Kwa hiyo, […]

Continue reading