UTUME KWA VIJANA 2
Sahaya G. Selvam, SDB
Yesu : Mfano Bora wa Utume kwa Vijana
Vijana wenyewe si matatizo, bali wanaweza kuwa na matatizo. Ni wajibu wa wanakanisa kuwasindikiza vijana na kuwasaidia ili wenyewe watatue matatizo yao. Huu ndio utume kwa vijana. Aliyetoa mfano mzuri kwa utume huu kwa vijana ni Yesu mwenyewe. Katika makala hii tutafakari jinsi Yesu mwenyewe alivyowasaidia vijana wawili, waliokuwa wamekata tamaa, kujenga matumaini na wenyewe kuwa mitume kwa vijana (wafuasi) wengine.
Tunapata mfano huu katika tukio la “Safari ya Kwenda Emau” (Lk 24:13-35)
Siku hiyohiyo, wawili kati ya wafuasi wake Yesu wakawa wanakwenda katika kijiji kimoja kiitwacho Emau, umbali wa kilomita kumi na moja kutoka Yerusalemu. Wakawa wanazungumza juu ya hayo yote yaliyotukia. (Lk 24: 13-14, Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa.)
Ningependa kufikiria kwamba hawa wafuasi wawili walikuwa vijana. Kadiri ya Sera ya Maendeleo ya Vijana katika nchi nyingi kama Tanzania, kijana ni mtu yeyote mwenye umri ya miaka […]