UTUME KWA VIJANA 7
Sahaya G. Selvam, SDB
Mambo Yatiayo Chachu katika Vyama vya Vijana
Katika makala iliyopita nilieleza kuhusu umuhimu wa vyama katika malezi ya vijana, niliorodhesha pia aina za vyama pamoja aina mbalimbali za shughuli zinazoweza kufanyika katika vikundi vya vijana. Katika makala hii ningependa kutaja na kueleza vipengele vichache vinavyosaidia kufanikisha vyama vya vijana.
1. Mfumo na Uongozi
Endapo chama cha vijana kitafanikiwa kutolea malezi ya jumla kwa vijana ni lazima kiwe mfumo mzuri, pamoja na uongozi bora. Ingawa mfumo wa chama unaweza kuwa tofauti kadiri ya malengo yake, hapa tunaweza kutaja mfumo wa jumla ambao unafaa kwa chama chochote kile. Kila chama kina wanachama wake, na viongozi wake ambao wanachaguliwa au kuteuliwa na wanachama. Uongozi unaweza kuundwa na watu kama watatu au watano kadiri ya mahitaji ya chama. Kuwa na watu wengi katika uongozi hakusaidii sana. Aidha, kila chama cha vijana lazima kiwe na mlezi, walau mmoja, […]